FAQ

Itachukua muda gani mzigo kufika?

Mzigo inategemea na nchi au mtandao ambao mzigo uo unatokea , kwa mfano mizigo inayotoka china inachukua siku 5 hadi 7 ikija kwa njia ya ndege na inachukua siku 30 hadi 45 ikija kwa njia ya meli , lakini ya Kutoka dubai inachukua siku 3 hadi 5 kwa ndege na siku 25 hadi 30 kwa meli , pia ukilipia order yako kwetu unakua unapata update(taarifa) ya mzigo wako kwa kila hatua ambayo mzigo wako unafikia.

Usalama wa pesa zako upoje?

Ukilipia kupitia sisi tunahakikisha pesa yako inapita njia sahihi na ikiwa kuna changamoto yoyote yamuuzaji kushindwa kufikisha mzigo kwako unaipata kwa uharaka zaidi , Tupo kwenye hii biashara zaid ya miaka 5 sasa na hatujawahi kumuangusha mteja ata mmoja kwenye usalama wapesa yake.

Itakuaje nikipata bidhaa tofauti na niliyoiagiza ?

Kazi yetu kuu nikuhakikisha mzigo unaoagiza ndio unaoupokea , kazi yako nikutupa maelezo yakutosha yatakayotusaidia kuuhakikisha mzigo wako ikiwa mzigo unahitaji ujuzi maalumu, kwa vitu vyakawaida kama simu ,laptop vyombo vya muziki na camera tunahakikisha tunakuletea kitu original kutoka brand Genuine za bidhaa hizo. Kila mzigo tunaonunua mtandaoni unahakikishwa ukiwa nchi iyo iyo unayotoka kabla yakuusafirisha kuja Tanzania ili iwe rahisi kuurudisha kwa muuzaji ukiwa na mapungufu yoyote.

Nahitaji kusafirishiwa tu muuzaji nimeshalimpa?

Huduma ya cargo tunaifanya kwa baadh ya nchi tu wasiliana nasi utuambia nchi ambayo mzigo wako upo ili tukupe maelekezo zaidi.